

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Mteule wa Uganda, Jenerali Yoweri Kaguta Museveni, amemtunuku nishani Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kwa kutangaza na kutambua ujasiri wake katika operesheni dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Sudan Kusini.
Katika hafla hiyo maalumu ya kijeshi, Rais Museveni alimpongeza Jenerali Muhoozi kwa uongozi madhubuti na mchango wake mkubwa katika kuhakikisha usalama wa kikanda, hususan katika mapambano dhidi ya makundi yenye misimamo mikali na yanayotishia uthabiti wa mataifa jirani.

Rais Museveni alisema kuwa mafanikio ya operesheni hizo ni matokeo ya ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na nidhamu ya hali ya juu iliyoonyesha na CDF Muhoozi katika kutekeleza majukumu yake.
Jenerali Muhoozi amekuwa akiongoza vikosi vya Uganda katika majukumu mbalimbali ya kijeshi ndani na nje ya nchi, ikiwemo operesheni za kudhibiti ugaidi, kulinda amani na kuimarisha usalama wa kikanda chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika.
Hafla hiyo imeelezwa kuwa ishara ya kutambua na kuthamini mchango wa majeshi ya Uganda katika kuhakikisha amani ya eneo la Maziwa Makuu na Afrika Mashariki.
The post Museveni Amtunuku Nishani Mwanaye CDF Muhoozi Kwa Ujasiri appeared first on Global Publishers.








