Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 17, 2026 amekagua na kuzindua shule mpya ya sekondari ya amali ya Majulai iliyopo katika kijiji cha Majulai, Kata ya Mwangoi, Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto.
Shule hiyo ambayo imejengwa kwa kupitia mradi wa SEQUIP na tayari imesajiliwa, ina walimu sita na wanafunzi 89 ambao walianza masomo Januari 13, 2026..
Mradi huo ambao umegharimu sh. milioni 584.28 ulianza kutekelezwa Oktoba 23, 2024 na hadi sasa umetumia sh. milioni 581.81 na kwamba sh. milioni 2.46 zilizobakia ni za angalizo, kukamilisha ujenzi wa tenki na kulipa mafundi.






