Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akimvalisha Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, vazi la utamaduni wa kimasai ikiwa ni ishara ya kumvika hadhi ya Laigwanan ambaye ni kiongozi wa kimila wa jamii ya kimaasai leo tarehe 22 Februari, 2026 wakati akikaribishwa kwa ziara zake za kikazi zilizoanza rasmi leo mkoani humo.
……
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya, akimvalisha Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba vazi la utamaduni wa Kimaasai ikiwa ni ishara ya kumvika hadhi ya Laigwanan kiongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai leo tarehe 22 Februari, 2026, wakati akikaribishwa kwa ziara zake za kikazi zilizoanza rasmi mkoani Arusha.
*Maana ya Laigwanan*
Laigwanan ni cheo cha heshima katika jamii ya Wamaasai, humaanisha kiongozi wa kimila au mzee mwenye ushawishi na uongozi wa kijamii. Kumvika mtu hadhi hii ni ishara ya:
•Heshima kubwa kwa mchango wake kwa jamii.
•Kukubalika na kuaminiwa na wazee wa kimila.
•Ushirikiano kati ya uongozi wa serikali na mila za asili.





