Pongezi hizo zimetolewa katika taarifa ya Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk wakati wakutoa taarifa inayoangazia maeneo yaliyokumbwa na changamoto ya vita na migogoro duniani katika kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva, Uswisi.
Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Turk alisema hatua iliyochukuliwa na Tanzania kuanzisha Tume ya kuchunguza kilichojiri Oktoba 29, kama hatua muhimu inayojali haki za binadamu
Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba, 2025 ilianza rasmi majukumu yake Desemba 2025, kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.







