Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni wakati sasa wa vijana wa Afrika kuongezewa nguvu katika uzalishaji wa zao la Kahawa ili Malengo ya uzalishaji katika sekta ya kahawa yafikiwe.
Rais Samia amesema hayo wakati akitembelea mabanda ya maonesho kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC), na wakati akitoa hotuba yake ya kufunga Kongamano la nchi 25 zinazolima Kahawa barani Afrika mjini Dar es salaam
Akilenga uongezaji wa thamani wa zao la Kahawa amesema utaongeza thamani ya zao hilo, kwani kwa sasa zao hilo linauzwa likiwa ghafi.na wanaonufaika ni walewanaolinunua , wanapata faida mara mbili zaidi ya mkulima ambaye amelima nakufanya kazi kubwa.
Rais Samia amesema Tanzania iko tayari kufundisha vijana wa Africa Kilimo kwani tayari Tanzania inayo programu ya BBT inayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri . Ambapo Tanzania imejikita katika Kilimo ufugaji na uvuvi.
Kwa habari ya soko la kahawa Rais Samia amesema Azimio la Biashara huru kwa Afrika lazima lisimamiwe vizuri “soko la Kahawa ilivyo kwa sasa ambayo ni kuuza Kahawa ghafi kwa bei ndogo Kisha inarudishwa Afrika ikiwa imepakiwa na kuuzwa kwa bei kubwa . Tanzania imeanza kupaki Kahawa ila ni vyema Afrika ikaungana kuhusu hili.”
Ametoa Rai kwa nchi za Afrika kulejesha hadhi ya zao la Kahawa na kuzitaka zikubaliane naye kuwa ifikapo 2035 asilimia 50 ya zao la Kahawa liongezewe thamani barani Afrika liuzwe likiwa limesindikwa.