Wenyeviti wa serikali za mitaa katika halmashauri ya jiji la Dar es saalam, wametakiwa kuunga mkono jitihada za Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anamtua Mama ndoo kichwani.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo wakati anafunga kikao kazi cha Dawasa na wenyeviti wa serikali za mitaa 159 wa kata 36 za wilaya ya Ilala.
Mpogolo amewaeleza wenyeviti hao kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dokta Samia katika kutatua kero ya maji kwa wananchi wa wilaya ya Ilala kutoa kiasi cha shilingi milioni 58 ili kuhakikisha tanki la maji la Pugu bangulo linakamilika na kuanza kufanya kazi ya kuhifadhi maji na kusambazwa.
Jambo ambalo linalotakiwa kupongezwa na wenyeviti hao na kufikisha ujumbe kwa wananchi wao ili kujua kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dokta Samia katika sekta ya maji ahadi ambayo aliiweka na kaitimiza kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025.
Amebainisha kuwa Mradi huo wa maji unakuwa mkombozi kwa wananchi kutokana na kukamilika kwake ili majimbo yaliyokuwa na changamoto ya maji kutoka dawasa wapate huduma hiyo kwani mifumo ya usambaji na ujazwaji wa banki la Pugu bangulo uko tayari.
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwataka wenyeviti wa mitaa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi ilo kwa Mkoa wa Dar es salaam litapoanza.
Na kusisitiza kujiandikisha kwa wingi ili wilaya ya Ilala iongoze katika kujiandisha na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi Mkuu utaofanyika mwaka huu kumchagua Rais, wabunge na madiwani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amewasisitiza wenyeviti kuwa viongozi shirikishi ili kupiga hatua kwenye maendeleo na kuendelea kumshukuru Rais Dokta Samia kwa kutoa fedha za miradi.
Aidha Kaimu Mtendaji Mkuu wa dawasa injinia Mkama Bwire amesema Dawasa inamshukuru Rais wa awamu ya sita Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuikwamua miradi mingi ya maji iliyosimama jambo linaloleta mabadiliko katika sekta ya maji nchini.