Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Latifa Khamis amesema kuwa moja ya mafanikio yao yaliyotokana na Uboreshaji wa mifumo ya Taarifa za Biashara na masoko ni pamoja na Biashara 36 za Kitanzania kusajiliwa katika Shirikisho la Kimataifa la Vituo vya Biashara (WTPF), huku ripoti 25 za bei za masoko zikisambazwa kwa wadau 179,728 kupitia Biashara App.
Latifa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wakati akielezea Mafanikio na mwelekeo wa Mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo Machi 13,2025 Jijini Dodoma.
Amesema kuwa hadi kufikia Machi 2025 mfumo wa TanTrade Biashara App umepata watumiaji 1,460.Trade Portal watumiaji 92,403 na watembeleaji zaidi ya 272,718 kutoka ndani na nje ya Nchi.
“Yafuatayo ni mafanikio yaliyotokana na kuboreshwa mifumo ya Taarifa za Biashara na Masoko, ambapo;Hadi Machi 2025 Mfumo wa TanTrade Biashara App umepata watumiaji 1,460.Trade Portal imefikia watumiaji 92,403, huku ikiwa na zaidi ya watembeleaji 272,718 kutoka ndani na nje ya nchi wanaopata taarifa za biashara”.
“Biashara 36 za Kitanzania zimesajiliwa katika Shirikisho la Kimataifa la Vituo vya Biashara (WTPF).Ripoti 25 za bei za masoko zimesambazwa kwa wadau 179,728 kupitia Biashara App, tovuti, na mitandao ya kijamii.Kanzidata ya wafanyabiashara imeboreshwa kwa kuongeza usajili wa kampuni 483 mpya”.
Aidha amesema kuwa Kampuni 85 za Tanzania zimekutanishwa na kampuni 31 za UAE kupitia Mkutano wa B2B ambapo kampuni 27 za ujenzi na Nishati zinaendelea na mazungumzo ya kuwa wakala wa bidhaa hizi Nchini.
“Tathmini ya Bidhaa za Tanzania Kampuni 85 za Tanzania zimekutanishwa na kampuni 31 za UAE kupitia mkutano wa B2B, ambapo kampuni 27 za ujenzi na nishati zinaendelea na mazungumzo ya kuwa wakala wa bidhaa hizo nchini.Kampuni ya Lico Global (Tanzania) imeingia makubaliano ya kuiuzia Tech Flyers Air Cargo LLC (UAE) tani 20 za karafuu zenye thamani ya USD 240,000”.
“Fursa za masoko katika nchi 50 zilifanyiwa tathmini na kusambazwa kwa wafanyabiashara kupitia tovuti, huku mwenendo wa bei na matarajio ya biashara katika nchi za Canada, Urusi, Ufaransa, na UAE ukichambuliwa ili kutoa maarifa muhimu kuhusu mwelekeo wa masoko”.
Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa Tanzania imepanua masoko ya bidhaa zake kupitia ushiriki katika maonesho ya Kimataifa kama DITF, Expo 2020 Dubai,CIIE, na maonesho ya Mbogamboga Expo Doha,ambapo wafanyabiashara wamepata mikataba ya kibiashara na masoko mapya.
“TanTrade imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kati ya 2020/21 – 2023/24 na tayari imeanza utekelezaji wa mpango wa 2024/25”.
“Tanzania imepanua masoko ya bidhaa zake kupitia ushiriki katika maonesho ya kimataifa kama DITF, Expo 2020 Dubai, CIIE, na Maonesho ya Mbogamboga Expo by Doha, ambapo wafanyabiashara wamepata mikataba ya kibiashara na masoko mapya. Vilevile, maboresho ya mifumo ya biashara kama TanTrade Biashara App na Trade Portal yameongeza upatikanaji wa taarifa kwa wafanyabiashara. TanTrade inaendelea kuimarisha mazingira ya biashara na kuwawezesha wafanyabiashara wa Kitanzania kushindana katika soko la kimataifa kwa ufanisi zaidi, kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa”.