NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Serikali ya awamu ya sita kupitia wizara yake ya mifugo na uvuzi imeanza kutekeleza azma yake ya mpango wa kuwasaidia wafugaji ambapo imetoa chanjo dozi 178,000 kwa halmashauri ya wilaya Kibaha na Bagamayo kwa ajili ya mifugo yao ikiwa ni moja ya chanjo zinazotolowe katika kampeni ya kitaifa kwa ajili ya uchanjaji wa mifugo hiyo ambayo lengo lake kubwa ni kuweza kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Operesheni kutoka kiwanda cha chanjo za wanyama cha Hester Biosciences Afrika Limited ambacho ndio kinatengeneza chanjo hizo Ms. Chistine Sokoine wakati wa halfa ya kukabidhi chanjo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pamoja na Bagamoyo.
Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba wamefanikiwa kutoa chanjo hizo zipatazo dozi 178,000 ambazo ni za aina mbili ikiwemo za Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP) na Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) ambazo zitatumika kuwachanja wanyama hao.
Aidha Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imewapa dhamana kupitia kiwanda hicho ikiwa ni miongoni mwa viwanda vya ndani kuzalisha na kusambaza chanjo hizo katika kampeni ya kitaifa ya kuchanja mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Ameongeza kwamba zoezi la usambazaji wa chanjo hizo limefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kukabidhi chanjo ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP) dozi zipatazo elfu 47,000 na ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) dozi elfu 60,000.
Kadhalika Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wameweza kukabidhi chanjo aina ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP) dozi zipatazo elfu 36,000 na ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) dozi elfu 35,000 ambazo zimemetolewa na serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji kuchanja mifugo yao.
“Chanjo hizi ambazo tumeweza kuzisambaza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pamoja na Halmashauri ya Bagamoyo jumla ni dozi 178,000 na kwamba utoaji wa chanjo hizi ni moja ya mgao wa chanjo katika kampeni ya kitaifa ambayo ipo chini ya serikali kupitia Wizara yake ya mifugo na uvuvi ili kuwasaidia wafugaji katika kuchanja mifugo yao na kuondokana na kutokomeza magonjwa mbali mbali,”amebainisha Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg.Raj Gera amesema kwamba lengo lao kubwa kama wawekezaji ni kuendelea kushirikiana na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha inawasaidia wafugaji kupata huduma ya uchanjaji wa mifugo yao kwa lengo la kuweza kudhibiti na kutokomeza magonjwa mbali mbali kwa wanyama.
Mkuu wa Idara ya kilimo,mifugo na uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Ms. Evelyne Ngwira wameishukuru sana serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuwapatia msaada wa chanjo kwa ajili ya mifugo mbali mbali ikiwemo, mbuzi, kondoo, ng’ombe, pamoja na mifugo mingine midogo midogo.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Bi. Regina Bieda amemshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuweza ktenga fedha nyingi kupitia Wizara ya mifugo na uvuvi ambazo zitakwenda kuwa ni mkombozi mkubwa wa wafugaji katika suala zima la kuwachanja wanyama wao na kuepukana na magonjwa mbali mbali.
Hivi karibuni Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 216 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 hadi mwaka 2029 ambapo kiwanda cha Hester Biosciences Afrika Limited ni miongoni mwa viwanda vya ndani ambavyo vimepewa jukumu kwa ajili ya utengeenzaji wa chanjo hizo zinazotumika kwa wanyama wa aina mbalimbali kama mbuzi,kondoo,Ng’ombe na wanyama wengine wadogo wadogo.