Wananchi wa vijiji vya Kijumo ,Kitendeguro na Rukurungo kata ya Bugandika wameipongeza serikali ya Dkt Samia Kwa kuleta kampeini ya msaada wa kisheria na kuunda timu inayoongeza uelewa Kwa jamii ya wananchi wa vijijini juu ya maswala ya kisheria hasa yanayohusu Aridhi na Hatimiliki.
Kupitia Kampeini ya msaada wa kisheria inayoendelea wilayani Missenyi kwenye maswala ya kisheria inayoendelea kutolewa jambo kubwa lililowagusa wananchi hao ni kuhusu Umuhimu wa kumiliki Hati miliki ya Aridhi jambo ambalo wamedai kuwa Iinaweza kupunguza migogoro ya Aridhi inayoendelea kwa sasa na namna Bora ya kuacha usalama wa familia ni kuwa na Hatimiliki ya eneo maeneo yao.
Afisa Aridhi na mipango miji na Vijiji wilayani Missenyi Deliqueen Lyimo akitoa Elimu ya kisheria kwa wananchi wa vijiji hivyo alisema kuwa mpango wa Serikali wa Wilaya hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata Hati miliki za Aridhi zao na Maeneo wanayoyamiliki ili kuyamiliki kisheria na kupata mikopo ya kufanyia biashara na kujiletea maendeleo.
Akitaja faida za kumiliki Hati miliki alisema kuwa changamoto nyingi za Aridhi zitapungua , wananchi watapunguza muda wa kwenda mahakamani kugombania Aridhi,wananchi watatumia hati zao kuomba Mikopo na kujiendeleza kimaendeleo pamoja na kuwasaidia warithi kutogombania Maeneo .
“Mama Samia aliona ni vyema mpate Elimu ya kisheria ili muweze kuondokana na changamoto ndogo ndogo na moja ya maswala ya Msingi ni kumiliki na kuwa na hati na hiyo itawaokoa sana na vijiji vitapata maendeleo sana kupitia hati hizo na baadhi mnagonbania mipaka lakini ukipima Aridhi Yako na kupata hati hautagombana na Jirani yako”alisema Lyimo
Kupitia timu hiyo wananchi wamewaomba wataalamu wa kisheria waliotumwa kutoa msaada wa kisheria kufikisha salamu kwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Raisi Samia kuwa wameipokea kampeini hiyo Kwa mikono miwili na wamefurahia Elimu na changamoto walizotatuliwa kupitia maswala ya kisheria walizotatuliwa
Ponsiani Peter (62) alisema kuwa swala la Kumiliki Hati miliki za viwanja na Maeneo zitapunguza changamoto na malalamiko kwani Moja ya changamoto kubwa za kisheria ni kugombania Aridhi na wengine wanagombania hata hatua 2 tu ambazo hauwezi kupanda kitu chochote.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kijumo Roberth Filederick alisema kuwa sasa ni muda wa vijiji kujianda kupeleka maombi Serikalini kwa ajili ya kupima Aridhi ili kujipatia maendeleo ambapo Amesema kuwa Elimu hii ni Fursa kwa wananchi wote wa vijijini kwani changamoto ya kutojua Sheria inachochea migogoro Mingi hivyo kampeini Hiyo imeleta mwanga mpya na matumaini mapya kwa wananchi wa vijijini.