Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), imepongezwa kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kupambana na rushwa Nchini.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ismail Ali Ussi ameyasem hayo jijini Dodoma wakati akikagua.mradi wa.shule ya sekondari ya Miyuji B,ulioenda sambamba na uzinduzi wa.klabu ya wapinga rushwa ya shule hiyo.
Amesema Takukuru wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na kuzuia rushwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini pia wamekuwa wakitoa elimu kwa shule za msingi hadi vyuo ambayo inawajenga wanafunzi kuikataa rushwa tokea wakiwa shuleni.
“Taasisi hii inahitaji pongezi kubwa sana kutokana na kazi nzuri wanayoifanya,tumejionea wenyewe miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezwa bila ya changamoto yoyote,”Ussi.
Naye Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema kata ya Miyuji inastahili.pongezi kubwa kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya ya kuupokea Mwenge wa Uhuru katika kata hiyo,ikiwemo kutoa eneo Kwa ajili ya kujengwa shule ya sekondari.
Mavunde amesema kitendo hicho ni kuonyesha uungwana katika kuunga mkono jitihada za serikali Katia suala zima la elimu kwa jamii inayotuzunguka.
“Tunawapongeza sana Kata ya Miyuji.kutokana na kazi kubwa wanayofanya,tuendelee na moyo huu wa kujitoa kwenye miradi ya serikali,”alisema Mavunde.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabiry Shekimweri,amemshkuru kiongozi wa mbio za.mwenge wa Uhuru kutokana na kuwazindulia mradi wa shule ya sekondari ambayo itatumika kwa wanafunzi wamaeneo hayo.