Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira leo tarehe 29 Aprili, 2025 ametembelea mafunzo ya watendaji wa Vituo (Waendesha vifaa vya Bayometriki na waandishi wasaidizi ngazi ya Kituo) katika Manispaa ya Sumbawanga kuona namna mafunzo hayo yanavyofanyika.
Mhe.Rwebangira amewataka watendaji hao kuzingatia mafunzo, ili wakatekeleze majukumu waliyoaaminiwa na Tume kwa umakini na uweledi. Mafunzo hayo ya siku moja yanatarajia kumalizia leo tarehe 29 Aprili,2025.
Tume ipo katika maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Pili na uwekaji wazi wa Daftari la awali mkoani Rukwa kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarehe 07 Mei, 2025 ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni.