Na Mwandishi Wetu.
Tume ya Ushindani (FCC), imesisitiza umuhimu wa kujenga uelewa wa pamoja kati ya wadau wa biashara ili kuhakikisha utekelezaji bora wa sheria na kukuza biashara bila malalamiko.
Akizungumza kwenye semina imewakutanisha wadau mbalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani William Erio amesema kuwa ni muhimu kwa wadau, wakiwemo wale waliopo ndani na nje ya nchi, kuelewa changamoto zinazokwamisha biashara na kushirikiana katika kutatua kero hizo.
Aidha, Erio ameongeza kuwa ni muhimu kwa nchi yetu kuendelea kuwa na taswira nzuri katika jamii ya kimataifa, hasa kwa kuzingatia kuwa biashara za kimataifa zinaathiri sana uhusiano wa kibiashara.






