Serikali ya awamu ya sita ikishikirikiana na sekta binafsi imedhamiria kuja na mpango wa kuanzisha vituo vya ukodishaji wa mitambo ya uchimbaji madini ambapo mitambo hii itaenda kuwa mwanga kwa wakulima pia.
Hayo yamesemwa na waziri wa madini Antony Mavunde wakati wa kilele cha kongamano la wachimbaji madini lililofanyika katika mamlaka ya mji mdogo Katoro mkoani Geita.
Mavunde alisema kuwa mitambo hii ya kukodi itaenda kuwa msaada mkubwa katika shughuli za uchimbaji hususani wachimbaji wadogo ambao walilazimika kununua mitambo mipya kwa gharama kubwa.
” Ukienda kwa wakulima, sio kila mkulima ana trekta la kulimia kwasababu ni ghalama kubwa kumililiki trakta wqchimbaji wadogo pia mmekuwa mkihangaika kupata mitambo sio kila mchimbaji mdogo anaweza kuwa na mitambo hii ndio maana serikali imekuja na mpango huu” alisema Mavunde
Aliongeza kuwa serikali imeshazungumza na sekta binafsi na kwamba wapo tayari kuanzisha kituo katika mkoa wa Geita ili kurahisisha kazi wachimbaji wadogo.