NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KLABU ya RS Berkane imeibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya leo kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Simba Sc na kuwa jumla ya matokeo ya 3-1.
RS Berkane imempa faida baada ya mechi ya kwanza ya fainali iliyopigwa Berkane nchini Morocco kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Katika mchezo wa leo Simba Sc iliweza kuutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Mutale.
Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, Simba Sc ilikuwa mbele kwa bao 1-0, huku kipindi cha pili wakiendelea kuutawala mchezo.
Simba Sc iliwafanya kucheza pungufu baada ya nyota wao Yusufu Kagoma kupewa kandi mbili za njano baada ya kucheza rafu.
RS Berkane wanachukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya tatu.