MRAJIS Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga,akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Bi.Happyness Olotu,akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA Ushirika Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ,Justin Mogendi,akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA Ushirika Wilaya ya Simanjiro, Moses Kaaya ,akizungumza wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
SEHEMU ya washiriki wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
…….
WANACHAMA wa Vyama vya Ushirika wa mazao ya Bustani Mkoani Manyara wanaojishughulisha na kilimo cha matunda na mbogamboga wamepatiwa mafunzo katika nyanja mbalimbali za uzalishaji wenye tija, masoko na uwekezaji kwenye shughuli zao.
Mafunzo hayo hayo yametolewa leo Juni 2, 2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi huo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Cheliga amesema moja ya kati ya kazi muhimu kwao ni pamoja na kuwajengea uwezo wanachama ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kujiongezea kipato.
Amesema lengo ni Wanaushirika kuongeza tija katika uzalishaji pamoja na kuiishi dhana ya ushirika, uzalishaji wa tija wakiwa shambani, masoko na uwekezaji kwenye shughuli zao.
“Natoa wito kwa jamii kujiunga na vyama vya ushirika kwa sababu ni nyenzo muhimu katika ushirikiano Pamoja na kuweza kujiongezea kipato,”amesema Cheliga
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AMCOS Mirerani, George Lyimo amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwaletea mafunzo hayo ambayo yamezidi kuwaongezea maarifa kwani Amcos yao ya Mirerani ni mpya.
“Kupitia mafunzo haya wanachama wataenda kupiga hatua na ni matumaini yetu serikali yetu ipo pamoja na sisi na sisi viongozi tuliopata mafunzo awamu ya kwanza na haya yamekuwa ni ya awamu ya pili, tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutufikia,” amesema Lyimo.
Afisa Ushirika Wilaya ya Simanjiro, Moses Kaaya amesema chama hicho kilianzishwa Februari mwaka jana ambapo kwa kipindi hicho wanachama wamepata mwitikio mkubwa kwani awali walikuwa 20 lakini kwa sasa wapo 100.
Amesema kupitia uongozi Madhubuti wameweza kuanzisha biashara ya mbolea kwa kuleta huduma karibu na wakulima.
Amesema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni mafuriko lakini Seriakli imeweza kutatua kwa kuchimba mfereji mkubwa na wakulima wanaendelea na shughuli za kilimo Januari hadi Disemba.