.jpeg)
Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Daniel Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam.
Naibu Mkuu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Daniel Mushi akizungumza na waandishi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Daniel Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam
Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo MUHAS, Idara ya Tafiti na Ushauri wa Kiutaalamu Profesa Bruno Sunguya akizungumza na waandishi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS Profesa Appolinary Kamuhabwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam.

*NI KATIKA KONGAMANO LA 13 LA MUHAS
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
SERIKALI imehimiza ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na taasisi za umma katika kuimarisha mifumo ya teknolojia inayotumika kwenye sekta ya afya, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha huduma bora, usalama wa taarifa za mgonjwa na matumizi sahihi ya rasilimali.
Imesema mageuzi ya teknolojia yameleta mwelekeo mpya duniani kote katika namna huduma za afya zinavyotolewa, hivyo Tanzania haiwezi kubaki nyuma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MuunganoTanzania, Kassim Majaliwa amesema hayo leo Juni 2025 wakati akifungua Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa mwaka 2025 Kampasi ya Mloganzila.
Kongamano hilo a siku mbili lenye kaulimbiu, “Kujipanga Upya kwa Mifumo ya Afya Afrika Kipaumbele kwa Ubunifu na Utafiti ili Kukabiliana na Changamoto Zinazobadilika za Afya Duniani” limewakutanisha washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Norway na Marekani.
“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuanzisha viwanda vya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Tuko tayari kushirikiana nanyi….ni maono ya Serikali kuweka misingi imara ili nchi yetu iweze kunufaika na teknolojia bila kuathiri ubora wa huduma, usalama na ulinzi wa taarifa,” amesema Majaliwa.
Pia, amewataka washiriki wa kongamano hilo kutoa mapendekezo ya Kisayansi kuhusu sera na miongozo ya matumizi ya teknolojia katika sekta ya afya, sambamba na kubaini mapungufu yaliyopo ili kusaidia kuandaa mikakati bora ya maendeleo.
“Ni muhimu kuhakikisha mifumo yetu inayotumia teknolojia inawasiliana na ushiriki wa sekta binafsi unaongezeka ili kupeana uzoefu na hamasa,” amesisitiza.
Aidha, Majaliwa ametoa maelekezo matano muhimu, ikiwa ni pamoja na wito kwa watunga sera na watafiti kufanya tafiti zenye matokeo chanya yatakayosaidia kuleta mageuzi katika sekta ya afya nchini.
Amesema matokeo ya tafiti yanapaswa kutumika katika kutengeneza sera bora na kuboresha mfumo wa utoaji huduma za afya nchini.
Pia ameelekeza wataalamu wa TEHAMA na wahudumu wa afya kuendeleza matumizi ya teknolojia ili kuboresha utoaji wa huduma za afya huku Vyuo vya mafunzo ya afya kuwekeza katika kuzalisha wataalamu mahiri kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo.
Amewaelekeza wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuwekeza katika vifaa tiba na huduma za uchunguzi ili kusaidia utambuzi wa mapema wa magonjwa Wananchi kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kuzingatia mitindo bora ya maisha ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, amesema wizara yake inajivunia mafanikio makubwa yanayoendelea kushuhudiwa katika sekta ya afya.
Amesema MUHAS ni miongoni mwa taasisi zilizofaidika na miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo.
“Tunaona fahari MUHAS kutambuliwa miongoni mwa vyuo vitano bora Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara,” amesema Prof. Mushi.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamevutia wataalamu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani kuja kutoa mafunzo nchini.
“Wizara ya Elimu iko tayari kushirikiana na MUHAS katika kuboresha mafunzo ya kada mbalimbali za afya,” ameeleza.
Naye, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema hotuba kuu ya kongamano hilo inajikita katika mageuzi ya mifumo ya afya barani Afrika kwa kuweka vipaumbele wazi na kukabiliana na magonjwa sugu yanayoikumba Afrika.
Ameeleza kuwa tafiti nyingi zinazowasilishwa zimefadhiliwa na taasisi za kimataifa na kwamba Serikali itaendelea kufadhili tafiti ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma, Prof. Bruno Sunguya, alisema jumla ya tafiti 200 (za mdomo na za bango) zitawasilishwa na watafiti kutoka Marekani, Norway, Kenya na Tanzania.
Amesema tafiti hizo zinagusa maeneo ya kimkakati kama vile magonjwa yasiyoambukiza (NCDs), afya ya mama na mtoto, na magonjwa ya kuambukiza kama vile malaria na kifua kikuu, kwa lengo la kubuni mbinu madhubuti zitakazowanufaisha wananchi.