Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), leo ameongoza kikao cha pili cha Tume ya Taifa ya Mipango Jijini Dodoma.
Prof. Mkumbo ameongoza kikao hicho kilichojadili Mandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Mmuda Mrefu (LTPP) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.