Wadau Wa Tasnia ya Urembo na Mitindo waombwa kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Kiwanda cha Urembo ( Beauty industry Tanzania) linalotarajiwa Kufanyika Septemba 05,2025 Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuziblog Muandaaji wa Tamasha hilo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Beauty industry Tanzania (BIT) Precious Joseph amesema Kumekuwa na Matamasha na Tuzo mbalimbali kwa baadhi ya Tasnia ikiwa sehemu ya Kuwatambua na Kuthamini michango yao ambapo katika tasnia ya urembo imekuwa bado.
Hata hivyo amesema Maonesho hayo yatafanyika kwa siku 1 tu huku likiwajumuisha Wana tasnia ya Urembo wote nchini ikiwemo watu wa Mapambo ya Uso,Kcuha,Nywele,Mikufu pamoja na Vipodozi .
Precious ameiomba Serikali kuwapa Motisha Kwa Wafanyabiashara katika Kiwanda cha Urembo na Mitindo nchini.
Kwa Upande Wake Miss Tanzania Halima Kopwe amewakaribisha Watu wote Kushiriki Maonesho hayo ili kutambulika kazi zao pamoja na Kujiongezea fursa za kujitangaza nje na ndani.
Ambapo amesema vizimba katika Maonesho hayo itagharamu shilingi 600000 kwa watakaolipia mapema.