Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa katika kipindi cha November 2020 hadi Aprili 2025 Mkoa wake umepokea jumla ya Shilingi Trilioni 1.131 kwaajili ya Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu na Miundombinu ya Barabara.
Ambapo amesema katika Sekta ya Afya zimetolewa Shilingi 146,340,236,113.41 na kupelekea ongezeko la Vituo vya Afya hadi 336 kutoka vituo 249,ongezeko la vituo vipya 87,Hospitali kutoka 3 hadi 11 mpya zikiwa 8,vituo vya afya kutoka 29 hadi 42 vipya vikiwa 13, Zahanati kutoka 217 hadi 283 na Huduma za Kibingwa mpya 5 ikiwemo upasuaji wa Pua,Koo na Masikio.
Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Julai 1,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya Mkoa huo kwa Kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Na kuongeza kuwa wagonjwa wa rufaa waliotibiwa ndani ya Mkoa wameongezeka hadi kufikia 478,002 ikilinganishwa na 128,305 baada ya huduma za kibingwa kuongezeka.
“Sekta ya Afya, Jumla ya Tshs 146,340,236,113.41 zimetolewa Vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka hadi 336 kutoka vituo 249 ikiwa ni Ongezeko la vituo vipya 87,Hospitali za Wilaya kutoka 3 hadi 11, mpya 8. vituo vya afya kutoka 29 hadi 42, vipya 13.zahanati kutoka 217 hadi 283, mpya 66 Huduma za kibingwa mpya 5 (Upasuaji wa pua, koo na masikio, mifupa na magonjwa ya ndani) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa zimeongezwa, hivyo wagonjwa wa rufaa waliotibiwa ndani ya Mkoa wameongezeka hadi kufikia 478,002 ikilinganishwa na 128,305”.
” Ongezeko la wagonjwa wa rufaa 349,697 (273%) ambao wangetibiwa nje ya Mkoa. Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoa 85% hadi kufikia 93% kimkoa. Vifaa tiba vya kisasa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (CTC – Scan, ECHO na ECG) ambapo awali wagonjwa walilazimika kwenda Hospitali za Rufaa ya Kanda Bugando (Mwanza) na Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili (Dar es Salaam).
Aidha katika upande wa Sekta ya Elimu amesema Jumla ya Shilingi 128,055,003,364.69 zimetolewa katika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za elimu ikiwemo ujenzi wa Shule za Awali,Msingi,Sekondari,Shule mpya za Amali na Shule mpya ya Bweni ya wasichana ya Kagera River.
“Sekta ya Elimu, Jumla ya Tshs 128,054,003,364.69 zimetolewa ili kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ya elimu ambapo zimejenga -Shule za awali na msingi kutoka 942 hadi 1,058, mpya 116 Shule za sekondari kutoka 224 hadi 292, mpya 68, zikiwemo shule mpya za amali (ufundi) tatu (3) na shule mpya ya bweni ya wasichana ya Mkoa ya Kagera River ambayo imegharimu zaidi ya Tshs. Bilioni 4.1”.
Mkoa huo wa Kagera una Wilaya Saba 7, Halmashauri 8, Tarafa 27, Kata 192, Vijiji 662, Mitaa 66 na Vitongoji 3,728. Aidha, Mkoa una majimbo 9 ya uchaguzi na dadi ya watu ikiwa ni 2,989,299 (Sensa 2022) na ni Mkoa wa 6 kwa wingi wa watu ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Mkoa huo hutegemea kilimo kukidhi mahitaji yao ya chakula na pia kama chanzo cha mapato.