Aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo Cha Kodi na Mjumbe wa Seneti ya Mkoa wa Dar es Salaam Mwaka 2021/2022, Amechukua na kurudisha fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Leo Tarehe 30/06/2025,
Amanzi ameingia rasmi Kugombea Jimbo Moja na Mbunge aliyemaliza Muda wake katika Jimbo Hilo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Taletale maarufu Babu Tale,
Amanzi ambae ndio kijana pekee aliyechukua fomu katika jimbo hilo akiwa na maono makubwa huku akijidhatiti kuwatumika wananchi pindi atakapopata nafasi hiyo ndani ya chama.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo ameona ni muda muhimu kuweza kulitumikia taifa lake
Amesema kutokana na utekelezaji wa ilani ya chama chini ya usimamizi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika majimbo mpaka nchi umepelekea kujitathimini na kuona anafaa kuweza kumsadia Rais kuisimamia na kutekeleza ilani ya chama kwa kuwatumikia wananchi.
“Kutokana na demokrasia iliyopo kwenye chama chetu imepelekea mimi kama kijana ambae nimejitathimini na kujipima lakini pia ninauzoefu wa uongozi ndani ya chama kuamua kuchukua fomu ili chama kikinipa ridhaa niweze kuwatumikia wananchi”,Amesema Amanzi.
Mpaka sasa Amanzi ni kijana Pekee aliyethubutu Kugombea Ubunge katika Jimbo Hilo la Morogoro Kusini Mashariki.