Dkt. Benjamini akiwa na familia yake wakati wa urudishaji fomu ya Ubunge
Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkufunzi wa Chuo cha Afya cha City College Dkt.Benjamin Mohamed amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha Mapinduzi kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni kwa kipindi cha mwaka 2025/2030.
Kada huyo amesema kwa sasa kazi iliyobaki kwake ni kusubiri taratibu za chama kwa ajili ya uteuzi wa nani atapeperusha bendera ya kugombea uchaguzi wa Octoba.
Dkt.Mohamed amerudisha fomu hiyo katika ofisi ya Wilaya ya CCM Kigamboni.
Mohamed amebainisha kwamba yeye yupo tayari kushirikiana na yeyote atakayeteuliwa na vikao vya juu vya CCM baada ya mchujo.
Amesema kuwa yeye kama kada wa CCM anachoangalia na kilichopo kwenye maono yake baada ya mchujo ni mustakabali wenye nguvu na afya wa chama chake cha CCM katika eneo la Wilaya ya Kigamboni.
Baada ya zoezi la mchujo na kura za maoni nitashikiana asilimiab100 kwa 100 yule atakaye teuliwa na CCM kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Kigamonio.
Aidha amesema ametumikia nafasi mbalimbali ndani ya Chama hivyo ana uzoefu wa kuweza kuwatumikia wananchi wa Kigamboni .