Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linashiriki katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na watakuwepo hapo kipindi chote cha maonesho ili kuwawezesha Watanzania.
Akifafanua hilo Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza Bi. Minaeli Kilimba ameeleza kuwa wamekuja kuwaelezea watanzania juu ya Mifuko ya Uezeshaji na namna wanavyoweza kunufaika nayo na kuutarifu Umma fursa zinazopatikana katika Mifuko hiyo.
Sambamba na hilo ameeleza kuwa wamekuja sabasaba kuvitangaza vituo vya uwezeshaji takribani 28 vinavyopatikana nchini ma huduma za kiuwezeshaji zinazopatikana latila vituo husika. ‘Niwaombe watanzania watembelee banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na kufika lilipo Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kuweza kupata taarifa za kiuwezeshaji kiundani zaidi’ aliongeza Bi. Minaeli.