Madakatari Bingwa kutoka korea ya Kusini wakiwafanyia Uchunguzi wangonjwa waliofika katika Hosptali Rufaa ya Mkoa wa Pwani –Tumbi kwenye Kambi ya matibabu ya Macho.
Madakatari Bingwa kutoka korea ya Kusini wakiwafanyia huduma ya Upasuaji wa mtoto wa jicho wangonjwa waliofika katika Hosptali Rufaa ya Mkoa wa Pwani –Tumbi kwenye Kambi ya matibabu ya Macho.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Hosptali Rufaa ya Mkoa wa Pwani –Tumbi akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Vision Care wa Tanzania Bi Jieun Park alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya Utambulisho.
……….
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa wa Macho kutoka Korea Kusini chini ya udhamini wa Taasisi ya Vision Care wanaendesha kambi maalumu ya upasuaji wa macho kwa njia ya matundu madogo kwa muda wa siku tano. Upasuaji huo umeanza kufanyika Julai 27 hadi Agosti 1, 2025.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani – Tumbi, Dkt. Amaan K. Malima ameushukuru uongozi MAXIMA wa Vision Care kwa ushirikiano wa karibu na wa mara kwa mara wanaoutoa kwa Hospitali na kuwakikishia wananchi wa Mkoa wa Pwani na Mikoa ya Jirani kupatiwa huduma bora na kuziishi ndoto za Mhe. Rais Dkt. Samia S Hassan.
Dkt. Malima aliendelea kwa kusema kambi hii maalum inaenda sambamba na mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa ndani ili kuwezesha huduma hii kuwafikia wananchi wengi zaidi hata Madaktari hawa Bingwa wa Korea wasipokuwepo.
Naye Mkurugenzi wa Mkazi wa Taasisi Vision Care Tanzania, Bi Jieun Park wakati wa utambulisho wake amesema upasuaji huu ni tofauti na uliokuwa unatumika hapo awali ambapo mgonjwa alikuwa anapasuliwa sehemu kubwa ili kuweza kutoa mtoto wa jicho. Bi. Jieun Park aliendelea kwa kusema kwamba upasuaji huu wa kisasa una faida nyingi kwa kuwa mgonjwa atapona kwa muda mfupi na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
“Kwasasa upasuaji unafanyika wa kisasa zaidi mgonjwa atapasuliwa sehemu ndogo tofauti na ilivyokuwa ikifanyika awali na kwamba katika Mkoa wa Pwani na Hospitali ya Umma Tumbi itakuwa Hospitali pekee, itakayokuwa inatoa huduma hii” amesema Bi Jieun Park.
Aliendelea kufafanua kwamba upasuaji huu mgonjwa atahudumiwa na kuruhusiwa siku hiyo hiyo kurejea nyumbani, atapona kwa muda mfupi na kuweza kuendelea na ratiba zake za kila siku.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Macho ya Hospitali ya Tumbi, Dkt Mathew Yinza ameeleza kwamba kambi hii itakuwa kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 28 Julai hadi tarehe 1Agosti,2025. Dkt Yinza amesema kwamba kambi hii itafanya uchunguzi mbalimbali kwa wenye changamoto ya macho kwa gharama nafuu na upasuaji wa mtoto wa jicho utakuwa bure. Na pia amewahimiza wanachi kujitokeza kwa wingi kuja kupata huduma hii.
Caption
Picha No 1,2,3
Madakatari Bingwa kutoka korea ya Kusini wakiwafanyia Uchunguzi wangonjwa waliofika katika Hosptali Rufaa ya Mkoa wa Pwani –Tumbi kwenye Kambi ya matibabu ya Macho.
Picha No 4na 3
Madakatari Bingwa kutoka korea ya Kusini wakiwafanyia huduma ya Upasuaji wa mtoto wa jicho wangonjwa waliofika katika Hosptali Rufaa ya Mkoa wa Pwani –Tumbi kwenye Kambi ya matibabu ya Macho.
Picha No 8na 9