Mwamvua Mwinyi, Pwani
Hawa Mchafu Chakoma amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Viti maalumu Mkoa wa Pwani baada ya kushinda kwa kupata kura 802 kati ya 2095 zilizopigwa.
Katika uchaguzi huo ambao umefanyika Julai 30 Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere Kwamfipa mjini Kibaha Mariam Ibrahim alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 645.
Nancy Mutalemwa alishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 449 akifuatiwa na Fatuma Uwesu aliyeambulia kura 71, Irene Makongoro (52), Sifa Mwaruka (44), Rehema Issa(26) na Rehema Mssemo (7).
Kura halali katika uchaguzi huo zilikuwa 2108, zilizopigwa ni 2095 na zilizoharibika ni tano.