
ARUSHA – Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe, usiku wa kuamkia leo Julai 31, 2025, amefanya sherehe ya send-off na mchumba wake mrembo, Yasmine, ikiwa ni hatua kuelekea katika tukio kubwa la ndoa yao inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Shughuli hiyo ya kifamilia na kiheshima imefanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu kutoka pande zote mbili.
Tukio hilo lilipambwa na burudani ya muziki, mavazi ya heshima na bashasha ya furaha kutoka kwa wanandoa watarajiwa, huku wageni wakisifia mpangilio na utulivu wa hafla hiyo.