NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
SERIKALI imesisitiza kuwa inaendelea kutoa kipaumbele kwa vijana kwa kutambua nafasi yao muhimu katika maendeleo ya taifa, huku ikiweka mazingira wezeshi ya kisera, mipango na mikakati mbalimbali ya kuboresha ustawi wao katika nyanja zote.
Kauli hiyo imetolewa leo, Agosti 6, 2025, jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu, wakati wa uzinduzi wa Mradi Shirikishi wa Kukuza Ustawi wa Vijana na Kuzuia Ukatili wa Kijinsia nchini (UVITA).
Mdemu amesema kuwa mradi huo unaenda sambamba na jitihada za serikali za kuimarisha ustawi wa vijana na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, huku akibainisha kuwa serikali imejipanga kuhakikisha vijana wanalelewa katika mazingira salama yanayowawezesha kufikia ndoto zao.
Aidha, aliongeza kuwa kupitia UVITA, vijana wataelimishwa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na namna ya kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Kwa upande wake, Profesa Neema Mori kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema kuwa mradi huo ni wa kipekee kwa kuwa unalenga kuimarisha mahusiano yanayolinda mipaka na maadili ya nchi, pamoja na kuchochea mabadiliko chanya ya fikra miongoni mwa vijana.
Mradi wa UVITA ni matokeo ya ushirikiano kati ya UDSM na Chuo Kikuu cha Sunset na unatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, ukihusisha vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 kutoka