

Katika kuadhimisha miaka 26 ya Siku ya Vijana Duniani, Jumuiya ya Vijana NCCR Mageuzi (JUVIMA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa JUVIMA Taifa, Ndugu Simeon Malisa wametembelea na kujifunza historia za viongozi mashuhuri Barani Afrika katika Kituo cha African Liberation Heritage.
Ni makumbusho ya urithi wa viongozi wa africa.
Wakiwa hapo walifanya yafuatayo;
1. Walitembelea maktaba maalumu yenye kumbukumbu nzuri za viongozi kitaifa na afrika.
2. Walipata elimu juu ya mbinu za kutumia kama viongozi vijana waliopo upinzani kuwasilisha hoja na sera kwa utawala bila kutweza utu wa mtu.
3. Walitumia jukwaa hilo kupeana mawasiliano na kujenga mahusiano na vijana wengine wenye akili waliofika kwenye makumbusho hayo ya afrika.
4. Walitumia fursa hiyo kueneza sera za jumuiya yao yaani JUVIMA na kualika maafisa pamoja na vijana kwenye chama.
Akizungumza baada ya matembezi hayo Malisa amesema safario hiyo imekuwa muhimu sana kwao n kwani kwenye kituo hicho wamejifunza mambo mengi kuhusu masuala ya siasa na kubwa zaidi ni kubadilishana mawazo na mawasiliano na wabobezi wa masuala mbalimbali ya kisiasa kwenye kituo hicho.