Kitendo cha kufanya mazoezi ya mwili kina msaada mkubwa katika mwili wa binadamu ikiwemo kujikinga na Magonjwa Yasiyoambukiza,kuweka utimamu wa mwili na akili pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
Aidha, mazoezi yanasaidia kuongeza hamu na nguvu za uzazi, pamoja na kuzuia magonjwa sugu kama vile shinikizo la juu la damu, kisukari, kansa ya ini na mapafu.
Kwa kuona umuhimu wa mazoezi hayo, Watumishi wa Wizara ya Afya leo tarehe 18,Agosti,2025 wameshiriki mazoezi ya pamoja katika viwanja vya Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Halikadhalika, mazoezi ya pamoja yanalenga kuhamasisha jamii na watumishi kwa ujumla kuwa na desturi ya kufanya mazoezi.