NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI wa Chuo cha Ufundi Stadi cha TURNBULL TECH kilichoko mkoani Iringa, Daudi Kingalata ametoa wito kwa vijana mkoani Iringa kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo mbalimbali ili waweze kuajiriwa au kujiajiri kwa urahisi kutokana na ujuzi atakaopata katika vyuo hivyo.
Kingalata ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa maonyesho ya Biashara yaliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa lringa yanayojulikana kwa jina la ‘Iringa Business Connect’ ya siku tatu yanayofanya katika viwanja vya Kichangani mjini hapa.
Amesema Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa vijana katika kuwawezesha kujiunga na vyuo vya Ufundi ili kujipatia ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri.
Alisema katika kuitikia wito Serikali wa vijana kujiunga na vyuo ametoa ushauri kujiunga katika chuo cha Turnbull ambacho kinatoa kozi mbalimbali na kuwapa ujuzi vijana wengi mkoani hapa unaoweza kukuweka kuwa miongoni mwa wanaotengeneza Pesa kila wakati.
Alisema kuwa vijana walioko vijiweni bila ujuzi wowote bado huwajachelewa kwani chuo hicho kinatoa mafunzo hadi muda wa jioni kwa lengo la kuwasaidia hata wale ambao bado wako makazini.
Alisema kuwa chuo hicho kinafanya juhudi za kusaidia kukuza na kuendeleza ubunifu wa vijana.
Kwa upande wake Secilia Godelo Mkufunzi wa chuo Tunrbul alisema kuwa chuo hicho kimewezesha vijana wengi wamewezeshwa na hadi sasa kujiajiri kutokana kuweza kumsaidia kijana kukuza na kuendeleza kipaji chake.
Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na Mafunzo na Elimu ya Ufundi Stadi katika chuo hicho ili kukuza uchumi wao kupitia ajira rasmi na zisizo rasmi.