Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma M. Abdallah, aliwasilisha mada kwa Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi za Umma.
Katika wasilisho lake, Bi. Abdallah aliwataka SOEs kuachana na urasimu na kuzingatia mbinu bunifu za kisasa ambazo zitarahisisha taratibu za kiutendaji na kuharakisha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Alisisitiza pia umuhimu wa kuanzisha mfumo thabiti unaojengwa juu ya utawala bora, uwazi, matumizi sahihi ya data, biashara endelevu na viashiria vya utendaji (KPIs) ili kuongeza tija na kuboresha matokeo ya huduma.
Kwa upande wake, Puma Energy Tanzania inajivunia mafanikio chanya yaliyopatikana kupitia mfumo wa nguzo tano unaojikita kwenye: Uongozi thabiti, Mageuzi ya sera, Miundombinu ya kidijitali, Nguvu kazi yenye wepesi na Utamaduni wa utendaji unaoendeshwa na matokeo.