Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, ametembelea na kufanya mazungumzo na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania ulioko Kampala nchini Uganda Agosti 15, 2025.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Ubalozi nchini Uganda Bi. Haikaeli Shishira, amemweleza Mkurugenzi Mkuu kuwa wanapata ushirikiano mkubwa kutoka Serikali ya Uganda na kwamba jitihada za Serikali ya Uganda katika kudhibiti vitendo vya rushwa zinaendelea. Aidha Bi. Haika ameipongeza TAKUKURU kwa hatua iliyofikiwa na Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugenzi Mkuu yuko nchini Uganda kuhudhuria kikao cha 29 cha Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika Mashariki – EAAACA.