Said Mwishehe,Michuzi TV
NI maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wanachama wa CCM,wakereketwa na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza katika Viwanja vya Tanganyika Packers kushuhudia uzinduzi rasmi wa kampeni za Chama hicho tawala.
Katıka viwanja hivyo ambavyo uzinduzi huo wa kampeni za CCM zinafanyika, kuna mabango mengi yenye ujumbe mbalimbali lakini miongoni mwa mabango yaliyovutia zaidi ni yale yaljyosomeka “CHAGUA SAMIA, CHAGUA CCM, KAZI NA ÜTÜ TUNASONGA, pamoja na lile bango maarufu ambalo linasema “OKTOBA TUNATIKI.”
Maelfu ya watu walianza kujitokeza tangu saa moja asubuhi ambapo mpaka muda huu saa saba mchana Uwanja wa Tanganyika Packers uko full house yaani toa Mguu weka mguu na hamu kubwa ya Wakazi wa Dar es Salaam ni kumuona kumsikia Mgombea Urais wa Chama hicho Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi.
Kama ambavyo tunafahamu CCM hainaga jambo dogo na katika uzinduzi wa kampeni hizo inaendelea kudhihirisha ukubwa na dhamira yake ya kuwatumikia Watanzania katika miaka mitano ijayo yaani 2025 hadi 2030 kupitia muongoza maono ya kuleta maendeleo ambaye ni Dk. Samia Suluhu Hassan.
Dk. Samia ameonesha kwa vitendo kazi hiyo anaiweza na yuko tayari kuwatumikia Watanzania kwa miaka mitano ijayo.
CCM inazindua kampeni zake leo Agosti 28 ikiwa ndiyo mwanzo wa safari kwenda kwa Watanzania kuomba kura sambamba na kuinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama hicho.
Hata hivyo tunafahamu Tume Huru ya Taifa ya Uchgauzi(INEC) ilitoa ratiba kuwa kampeni za uchaguzi Mkuu 2025 Kwa Tanzania bara zitaanza Agosti 28 hadi Octoba 28 na kwa upande wa Tanzania Zanzibar kampeni zitaanza Agosti 28 na kumalizika Oktoba Octoba 27 mwaka huu.
Hivyo kwa mujibu wa ratiba hiyo CCM imeanza kampeni zake leo na kutarajia kuhitimisha Oktoba 28 mwaka huu.