NA VICTOR MASANGU
Katika kuunga mkono juhudi mbali mbali zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita. Dkt. Samia Suluhu Hassan hususan katika kundi la vijana uongozi wa chuo cha Furahika education College (FEC) kilichopo Jijini Dar es Salaam inatarajia kuwapatia mafunzo ya fani mbali mbali kwa vijana wapatao 300 ambapo watapataa fursa ya kusoma masomo tifauti kwa kipindi cha mwaka mmoja bure bila malipo yoyote.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mkuu wa chuo hicho cha Furahika Dkt. David Msuya amesema kwamba lengo kubwa la mafunzo hayo ni kwa aajili ya kuweza kuwasaidiaa vijana kuondokana na wimbi la matumizi yaa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika maakundi mabaya.
Msuya amebaainisha kwamba chuo chao kimeamua kushirikian bega kwa bega na serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalum katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa mafunzo hayo bure kwa lengo la kuwasaidi vijana kupat ujuzi n maharifa mbali mbali bila malipo yoyote.
“Chuo chetu cha Fuhahika kwa sasa tumeamu kuung mkono juhudi za serikali y wamu y sit n kwamba tunshirikiana na Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum na hii yote ni kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu kupata mafunzo na ujuzi wa fani mbali mbali ili wasiweze kujingize katika makundi mabaya ikiwemo kujihusisha na madawa ya kulevyaa pamoja ngono,”amebaainish Dkt Msuya.
Kaimu mkurugenzi huyo amebainisha kwamba vijana hao 300 aambaao wanatarajia kuanza rasmi mafunzo hayo mwezi 0ctoba mwaka huu na kubainisha kwamba zoezzi la usahili kwa wanafunzi hao unatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 2 mwezi wa tisa kupitia tovuti ya chuo au kwenda katika ofisi zao zilizopo maeneo ya Buguruni malapa.
Aidha Msuya amezitaaja badhi ya kozi ambazo watafundishwa vijana hao ni pamoja na ufundi selemala, mapishi, kompyuta (ICT) , upigaji wa picha,masuala ya bandari,kozi na ususi,kozi ya udereva, biashara na masoko, kozi ya utalii pamoja na fani nyingine mbali mbali za uongozi katika mambo ya kibiashara.
“Pia amewahimiza wazazi, walezi pamoja viongozi wa chama wakiwemo wale wa jumuiya kuhaakikisha wanawahimiza vijanaa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupta ujuzi mbali mbali naa hatimaye kuweza kujiajiri na kuondokana na kuwa tegemezi,”amebinisha Msuya.
Katika hatua nyingine Msuya amebainisha kwamba watapatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo gharama zake zote zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zimetolewa na wafadhili kutoka nchini Ujerumani kwa lengo la kuweza kuwakomboa vijana kutoka Tanzania bara na visiwani ambao wameshindwa kujiendeleza na wengine hawana ujuzi wowote.