
Maelfu ya wananchi wamejitokeza kuhudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika viwanja vya Tumbaku, mkoani Morogoro, tarehe 29 Agosti 2025.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa chama, wafuasi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ambapo kulikuwa na shamrashamra, nyimbo za kampeni na mabango ya kuhamasisha kura.