Afisa maendeleo ya jamii kutoka ASPA, Albert .Mbwambo wakati akizungumza katika.zoezi la kutoa matibabu kwa mnyama punda katika mnada huo.

Afisa elimu ustawi wa wanyama ASPA ,Diana Msemo akimpatia dawa ya minyoo mnyama punda katika mnada huo uliopo jijini Arusha.




……………..
Na Happy Lazaro, Arusha
Shirika la ASPA kwa kushirikiana na shirika la BROOKE East Afrika kwa pamoja wameshirikiana katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kumlinda na kumthamini myama punda pamoja na kutoa matibabu mbalimbali ikiwemo dawa ya minyoo.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Afisa maendeleo ya jamii kutoka ASPA, Albert .Mbwambo wakati akizungumza katika.zoezi la kutoa matibabu kwa mnyama punda katika mnada wa Mirongoine uliopo kata ya Mirongoine mkoani Arusha .
Amesema kuwa ,Shirika la ASPA wamekuwa wakitembelea minada mbalimbali na kuweza kutoa elimu namna ya kumtunza na kumdhamini myama punda kwani ni mnyama ambaye amesahaulika katika jamii kwa muda mrefu.
“Kila tukija huu mnada huwa tunatoa huduma kwa punda zaidi ya Mia tano ambapo kila.soko huwa wanakuwa na punda zaidi ya elfu mbili na huduma hiyo ni mwendelezo katika minada mbalimbali “amesema .
Aidha mradi huo wa ustawi wa myama punda unatekelezwa na shirika la ASPA kwa kushirikiana na wafadhili ambao ni BROOKE East Afrika ambapo tangu kuanza kwa mradi huo kumekuwa na mafanikio makubwa sana .
Amesema kuwa , wanafanya kazi nchi nzima hususani katika maeneo ya wafugaji ikiwemo mnada wa Meserwni,Monduli, pamoja na Simanjiro ambapo wamekuwa wakitoa elimu pamoja na kutibu majereha mbalimbali ya punda yanayotokana na kubebeshwa mzigo mzito pamoja na kupewa dawa ya minyoo.
“Mbali na kutoa huduma hiyo pia katika minada hiyo tumeweza kuwajengea hifadhi maalumu ambayo inawasaidia punda kupumzika na kunywa maji wakati wananchi wakiendelea kufanya shughuli zao.”amesema .
Naye Afisa elimu ustawi wa wanyama ASPA ,Diana Msemo amesema kuwa linajihusisha na utetezi wa mnyama punda kwani ustawi wao ipo chini kuliko wanyama wengine .
Amesema kuwa, mnyama punda asilimia karibu 70 ya mizigo ambayo imekuwa ikipelekwa mnadani inapelekwa na punda ambapo wakati mwingine hubebeshwa mzigo mkubwa ambao humsababishia kupata vidonda ambapo ni kinyume cha sheria .
“Punda amekuwa akikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo mikubwa na kuwasababishia vidonda,kutopewa dawa ya minyoo pamoja na kutopewa chakula kwa wakati pindi wanapokuja mnadani hali inayowasababishia wao kuzeeka wakiwa vijana na wakati mwingine wanazibwa mdomo ili wasiokote takataka barabarani.”amesema .
Aidha ametaja changamoto nyingine inawakabili wanyama hao kuwa ni pamoja na ugonjwa wa pepopunda hali inayowasababisha kufa haraka .
Naye Afisa kilimo na mifugo kata ya Muriet,Sweka Saakumi amesema kuwa wanalishukuru shirika hilo kwa namna ambavyo limewajengea uwezo wa kumtunza mnyama punda na hatimaye wafugaji kuweza kumdhamini punda pamoja na kupatiwa matibabu .
“Kwa Tanzania hakuna chuo kinachofundisha maswala ya kumhudumia punda kwa ujumla hivyo kitendo cha shirika hilo kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji kimesaidia sana kwani wanamthamini mnyama huyo na kumtunza”amesema.
Nao baadhi ya wananchi ambao ni wafugaji wa punda,Namnyak Liki na Meng’oriki Kispanl wanalishuruku shirika hilo kwa namna ambavyo limekuwa likiwasaidia kuwapatia punda matibabu pamoja kuwajengea sehemu maalumu ya kupumzikia punda hao huku wakipata maji ya kunywa.