
Zanzibar, 30 Agosti 2025 – Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo amechukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Dkt. Mwinyi aliwasili katika ofisi za ZEC akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo:
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC)
Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari (MNEC)
Katibu Mkuu wa UWT, Suzan Peter Kunambi (MNEC)
Pamoja na wananchi na wafuasi wa CCM waliojitokeza kumshuhudia.
Hatua ya Dkt. Mwinyi kuchukua fomu inamfanya kuwa miongoni mwa wagombea rasmi wa CCM kuelekea uchaguzi wa Urais wa Zanzibar, huku chama hicho kikiendelea na mchakato wa kidemokrasia kuhakikisha ushindani na upatikanaji wa mgombea wa kupeperusha bendera yake.