Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi ( wa tatu kushoto) alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Beach jijini Mwanza kumwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza, Septemba 11, 2025. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Michael Lushinge (Smart) na wa tano kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Jim Yonaz. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandishi wa Mitambo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Hassan Temba (kulia) alipotembelea banda la maonesho la TPDC alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa kufungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza, kwenye hoteli ya Malaika Beachi jijini Mwanza, Septemba 11, 2025, Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na uratibu, William Lukuvi na Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TPDC, Francis Mwakapalila. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandishi wa Mitambo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Hassan Temba (kulia) alipotembelea banda la maonesho la TPDC akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza, kwenye hoteli ya Malaika Beachi jijini Mwanza, Septemba 11, 2025, Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TPDC, Francis Mwakapalila. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akimsikiliza Mhifadhi kutoka Wakala wa Hifadhi za Misitu Tanzania (TFS) Kombo Siwa alipotembelea banda la maonesho la TFS alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliani, Tathimini na Kujifunza, Septemba 11, 2025, Kulia kwake ni Waziri wa chi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza, kwenye Hoteli ya Malaika Beach jijini Mwanza Septemba 11, 2025, (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi baada ya kufungua Kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathimini na Kujifunza, kwenye hoteli ya Malaika Beachi jijini Mwanza, Septemba 11, 2025, Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Jim Yonazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………….
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa shughuli za ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu ya kuliwezesha Taifa kufanikisha na kufikia malengo mbalimbali ya kimaendeleo.
Amesema kuwa ni ukweli usiopingika wadau wote na jamii kwa ujumla wakiwa na uelewa wa pamoja kuhusu shughuli za ufuatiliaji na tathmini matokeo ya haraka yatapatikana.
Amesema hayo leo Alhamisi (Septemba 11, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika katika ukumbi wa hotel ya Malaika Beach jijini Mwanza.
Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia ya kuimarisha upimaji wa utendaji wa Taasisi za Umma, uwajibikaji na kuongeza kasi na uwazi katika kutoa huduma na ustawi wa wananchi kwa ujumla.
“Shughuli za ufuatiliaji na tathmini zinahusisha ukusanyaji, uchambuzi na upimaji wa taarifa kuhusu shughuli zilizopangwa, utekelezaji na matokeo yaliyopatikana. Serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya shughuli hii katika vipindi mbalimbali”.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Idara zote zenye dhamana zihakikishe zinakamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa upande wa Serikali zote mbili ili kuwezesha kutungwa kwa Sheria inayokwenda kuongoza Ufuatiliaji na Tathmini.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mamlaka ya Serikali Mtandao kukamilisha Maandalizi ya Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa kielektroniki. Utakuwa Mfumo Mkuu wa Mifumo yote ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji ndani ya Serikali lengo ni kuweza kuzifuatilia idara za Serikali vizuri, na utawezesha viongozi, watoa maamuzi na wananchi kupata taarifa na takwimu sahihi na kwa muda.
“Watendaji wakuu wote tumieni taarifa zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji na tathmini ili mfanye maamuzi na kuweka mikakati imara ya kuhabarisha umma juu ya matokeo ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa uhakika zaidi”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa rai kwa Chama cha Wataalamu wa Tathmini Afrika (AfrEA), kuendelea kuzilea TanEA (Tanzania) na ZaMEA (Zanzibar) kwa kuzipa uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwaongoza katika mabadiliko ya kiteknolojia ya utunzaji takwimu na ufuatiliaji.
“TanEA na ZaMEA, endeleeni kujiimarisha na kuongeza kasi ya kuwaunganisha wadau wote muhimu kwa lengo la kubadilishana mawazona uzoefu au kujadili mbinu mpya na bora za zitakazowawezesha kuwafikisha kufanikiwa katika kufanya ufuatiliaji na tathmini wake”.
kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi amesema kuwa katika jitihada zakuimarisha Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini nchini,Ofisi ya Waziri Mku kwa kushirikiana na Mamlaka Mtandao – eGA imefanikiwa kuanza ujenzi wa mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki waufuatiliaji na tathmini “Government Wide Electronic Monitoring and Evaluation System”ambao utapokea taarifa kutoka mifumo mingine na kuzichakata na kuwezesha maandalizi yataarifa ya utendaji wa Serikali.
“Uwepo wa Mfumo huo utawezesha kupokea data, kuzichakata, kuzitafsiri kwa wakati na kuiwezesha Serikali katika ngazi zote kutumia takwimu sahihi katikakupanga, kuboresha afua zinazotekelezwa nakuamua kwa usahihi”.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliweka msingi imara wa kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini kwa kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali
Amesema kiwa Idara hiyo imeendelea kuwa idara nguzo na muhimu katika kuchangia na kuendeleza juhudi za kuboresha utaalamu wa kufanyia tathmini nchini ambayo imewezesha mashirika ya umma na taasisi mbalimbali kujifunza kutoka katika idara yetu hiyo. “Na tunaamimi kwamba si tu ndani ya nchi bali imeendelea kuwa mwanga hata nje ya nchi, hii ndio nia yetu ya kuifanya iwe kituo cha kujifunza na maarifa”
Kwa Upande wake Muwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Suzan Ngongi amesema kuwa uwazi na uwajibikaji umeiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu pamoja na mipango ya kupambana na umasikini “Jitihada hizi zimeifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati”