
KIGOMA – Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemvalisha kofia ya chama hicho mwanachama mpya, Ndugu Said Bakema Rashid, aliyewahi kuwa kiongozi na mratibu wa ACT-Wazalendo kwa mikoa mitano ikiwemo Kigoma.
Bakema alitangaza kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Septemba 14, 2025, kwenye Uwanja wa Katosho, mkoani Kigoma.