Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Jumanne Septemba 16,2025 ameendelea na mikutano yake ya Kampeni za kusaka kura za ushindi akianzia kufanya mkutano katika viwanja vya Bokwa Wilaya ya Kilindi,na baadae akaelekea wilaya ya Muheza na kuwahutubia Wananchi katika uwanja wa Jitegemee,mkoani Tanga.
Akiwa katika mikutano hiyo ya kampeni,Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo ya kuwanadi Wagombea Ubunge na Madiwani wa mkoa huo.
Dkt. Nchimbi anahitimisha kampeni zake leo ndani ya wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho 2025-2030 kwa Wananchi, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025