Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya mikutano ya kampeni visiwani hapa mjini Unguja.
Katika mikutano hiyo ya kampeni itakayoanza kesho, maelfu ya wananchi wakiwa na shahuku kumsikiliza akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Tayari Dk. Samia ameshafanya mikutano yake katila mikoa 10 ambayo ni Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe, Singida, Tabora, Kigoma na Songwe.
Katika mkutano huo, Dk. Samia alivitaja vipaumbele mbalimbalk ambayo serikali yake itavitekeleza pindi akipewa ridhaa na wananchi kuongoza taifa.
Tangu Dk. Samia alipoingia madarakani katika kipindi cha miaka minne, mafanikio mbalimbali yamepatikana yaliyowezesha kuimarisha uchumi wa wananchi.
Pia, serikali yake imeendelea kuwezesha wananchi wa pande zote mbili za Muungano kiuchumi na kijamii.