
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 17, 2025 amemnadi Mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja – Zanzibar.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, Dkt. Samia alisisitiza mshikamano na mshikikano wa kitaifa, akiwataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwa uongozi wa nchi zote mbili – Tanzania Bara na Zanzibar.
Aidha, amesisitiza dhamira ya chama hicho kuendeleza maendeleo, kuimarisha umoja na kulinda amani ya taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.