
Miili ya Masista wa Kanisa Katoliki waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, imewasili jijini Dar es Salaam na kupokelewa katika Makao ya Masista Boko.
Tukio hilo limegubikwa na simanzi kubwa, huku waumini, ndugu, jamaa na viongozi wa Kanisa wakikusanyika kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Aidha, Kanisa Katoliki limeeleza kuwa litatoa ratiba rasmi ya ibada na maziko, ambapo misa maalum ya kuwaombea marehemu itafanyika kabla ya safari ya mwisho ya kuwapumzisha.
Ni tukio lililowagusa waumini wengi, kwani Masista hao walihusiana kwa karibu na jamii kupitia huduma za kiroho, elimu na afya.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.