Picha za Matukio mbalimbali ya Maadhimisho ya siku Faru Duniani ambapo leo tarehe 22 Septemba 2025 Maafisa na Askari wa Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Karatu, wadau wa Uhifadhi na Utalii na Wananchi wameungana katika Mbio za kilomita 5 katika mji wa Karatu zenye lengo la kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa Mnyama Faru.
Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Faru ni “Tuhakikishe aina tano za Faru waliopo duniani wanaishi”
Katika maadhimisho ya Siku ya Faru Duniani Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inafanya shughuli mbalimbali ikiwepo kutoa elimu ya uhifadhi wa Faru kwa jamii, kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, maonesho ya uhifadhi wa Faru pamoja na Michezo mbalimbali yenye lengo la kuhamasisha uhifadhi wa Farm.