
Uongozi wa Shule ya Sekondari Makumbusho iliyopo Wilaya ya Kinondoni imemuondoa kazini Mwalimu Felix Msila kutokana na tukio la kutoa adhabu ya viboko kikatili kwa Mwanafunzi wa kidato cha Pili, Khatib Salim, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiahidi kuchukua hatua zaidi.
Tukio hilo lilitokea Alhamisi Septemba 18, 2025 na baadaye picha mjongeo zilisambaa katika makundi
mbalimbali ya WhatsApp.
Kwa mujibu wa barua ya shule hiyo, Mwalimu Msila Felix amefukuzwa kazi kuanzia Septemba 19, 2025 na Mkuu wa Shule ya Sekondari Makumbusho.
“Kufuatia tukio ulilolifanya la kutoa adhabu kikatili kwa
Mwanafunzi wa kidato cha Pili Khatib Salim siku ya Alhamisi Septemba 18, 2025 bila kuzingatia waraka wa elimu namba 24 wa mwaka 2002 kuhusu utoaji wa adhabu ya viboko shuleni,” imeeleza barua hiyo na kuongeza.
“Uongozi wa shule kwa kushirikiana na Kamati ya Wazazi umekufukuza kazi rasmi kuanzia leo Septemba
19, 2025.”