
Uongozi wa Klabu ya Simba umetangaza rasmi kuachana na kocha wake mkuu, Fadlu Davids, baada ya pande zote kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba.
Davids, ambaye alijiunga na wekundu hao wa Msimbazi mwaka jana, amehudumu kwa muda wa mwaka mmoja na kufanikisha timu hiyo kufuzu hatua mbalimbali za michuano ya ndani na kimataifa.
Simba imemshukuru kocha huyo kwa mchango wake ndani ya klabu na kumtakia kila la heri katika safari yake mpya ya ukufunzi. Hata hivyo, klabu haijataja rasmi mrithi wake atakayekaimu nafasi hiyo kwa sasa.