Tanzania yaendelea kutekeleza Vigezo vya Kimataifa vya EITI kikamilifu
Uwazi wa Mikataba katika sekta ya uziduaji waanza kutekelezwa.
GEITA
Katika maonesho hayo yaliyofunguliwa tarehe 22 Septemba, 2025 na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.
Imeelezwa kwamba, tangu Tanzania ijiunge na Asasi ya Kimataifa ya EITI iliyopo nchini Norway, TEITI imeendelea kutekeleza kikamilifu vigezo vya Kimataifa vya EITI vya mwaka 2023 pamoja na Sheria ya TEITA, 2015 ambapo katika tathimini ya umoja wa EITI ulifanyika hivi karibuni Tanzania imeendelea utekelezaji wa vigezo vya EITI kikamilifu.
Hayo, yameelezwa leo Septemba 23, 2025 na Meneja Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji kutoka Taasisi ya TEITI – Bw. Erick Ketagory.
Bw. Ketagory amesema kuwa, katika kipindi cha kuanzia 2009 hadi 2025 TEITI imetoa ripoti 15 za ulinganishi wa malipo ya Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na mapato ya Serikali ambapo ripoti ya 15 ya TEITI kwa mwaka 2022/2023 iliwekwa wazi mwezi Juni, 30 mwaka 2025.
Kwa upande mwingine, Bw. Ketagory amesisitiza kuwa utekelezaji wa Takwa la uwekaji wazi wa Mikataba ambayo Serikali imeingia na kampuni za sekta ya uziduaji imeanza kutekelezwa ambapo Mikataba hiyo imewekwa wazi kupitia tovuti ya TEITI.
Tunawakaribisha wananchi wote Mkoani Geita kutembelea banda la TEITI ili kujifunza majukumu ya TEITI na namna ya kutumia takwimu zinazotolewa na tipoti za TEITI, “alisisitiza Bw. Ketagory”
Taarifa na Ripoti za TEITI zinapatkana kupitia: www.teiti.go.tz