
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), Annalena Baerbock ameuambia mkutano wa suluhisho la mataifa mawili uliofanyika makao makuu ya umoja huo jana Jumatatu: kuwa “nchi-dola huru ya Palestina lazima ianzishwe”.
Baerbock akaongeza: “hali halisi ya watoto wa Ghaza ni vita na uharibifu. Wengi wameuawa huko Ghaza bila ulimwengu kujua majina yao.”
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amefafanua katika hotuba yake hiyo kwa kusema: “ulimwengu umewaangusha watoto wa Ghaza. Watoto wote katika Mashariki ya Kati wanastahili kuishi”.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Baebock amesema: “tunahitaji usitishaji vita wa haraka na bila masharti huko Ghaza. Hamas lazima iwaachilie mateka wote mara moja na bila masharti”.
Rais huyo ni Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani amewaeleza washiriki wa mkutano wa suluhisho la nchi-dola mbili: “hali ya kutisha ya Gaza inaonyesha kwamba hatuwezi kuruhusu uharibifu kama huo utokee tena. Hali ya Ghaza haikubaliki na vita lazima vikome”.
Baerbock amesisitiza kwa kusema: “nchi huru na endelevu ya Palestina lazima ianzishwe. Hamas inapaswa kuweka chini silaha zake na kuhitimisha utawala wake huko Ghaza”. Rais wa sasa wa Palestine ni Mahmoud Abbas
MADEREVA 15 WAKAMATWA, LESENI 7 ZAFUTWA KATIKA OPERESHENI KALI YA TRAFIKI….