
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, ameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kumwaga Hayati, Askofu Mkuu Novatus Rugambwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, akisaidia na Askofu Mkuu Msaidizi wa Vatican Edigar Pena Para, Maaskofu wakuu wengine, maaskofu na Mapadre.
Mwili wa Hayati Novatus Rugambwa, unatarajiwa kuagwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu Jimamosi Septemba 27, 2025 na atazikwa siku ya Jumatatu Septemba 29, 2025 katika Jimbo Katoliki Bukoba
Hayati Novatus alizaliwa Oktoba 08, 1957.
Aliwekwa Daraja Takatifu ya Ushemasi 05 Januari 1986 na Hayati Nestorius Timanywa, Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba.
Aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Upadre Julai 06, 1986 na Hayati Askofu Nestorius Timanywa.
Februari 06, 2010 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict XVI kuwa Askofu Mkuu wa heshima wa Tagaria.
Na Aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Uaskofu Machi 18, 2010 na Mwadhama Tarcisio Kardinali Bertone SDB, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican.
Septemba 16, 2025 Mwenyezi Mungu alimwita kwake baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.
Raha ya Milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani.
Amina