………
NA DENIS MLOWE, IRINGA
BAADA ya kimya cha Muda Fainali ya mashindano ya kombe la Vunjabei 2025 itachezwa leo kati ya Kising’a fc dhidi ya Mgela Fc.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege ambapo kabla ya mchezo huo kutakuwa na mchezo wa utangulizi kati ya timu ya Chama cha Mpira dhidi ya timu ya jeshi la Polisi.
Akizungumza na mwandishi , Katibu wa mashindano hayo, Pastor Kwambiana alisema kuwa licha ya Fainali hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali hili kuweza kuifanya iwe na mvuto zaidi na kuwataka mashabiki wa soka kufika kwa wingi kushuhudia mchezo huo.
“Shughuli itapambwa na matukio/burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa utangulizi utakao husisha timu ya CHAMA CHA MPIRA dhidi ya timu ya JESHI LA POLISI.” Alisema
Aliongeza kuwa Mchezo utakaoanza majira ya saa nane kamili mchana na baadaye majira ya saa kumi kamili jioni utachezwa mchezo wa fainali hiyo kati ya KISING’A FC dhidi ya MGERA FC.
Hivyo wapenzi, wadau, mashabiki na watazamaji wa michezo mnakaribishwa sana kuja kushuhudia nani ataibuka na milioni 10 zilizoko mezani kwa ajili ya bingwa na kudhaminiwa na mkurugenzi wa kampuni ya VunjaBei Fred Ngajilo.
Mshindi wa pili ataibuka na kiasi cha sh milioni 3 na mshindi wa 3 ataondoka na milioni 2.
Aidha alisema kuwa kutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora wa mashindano,timu yenye nidhamu, mwandishi bora katika vipengele vitano kama tv,blog,gazeti, mitandao na radio.