Na Sophia Kingimali.
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema wahandisi wasiofanyakazi kwa weledi na uadilifu na nidhamu wanapaswa kufutiwa leseni zao na kutopewa miradi yeyote ya kijamii.
Hayo ameyasema leo Septemba 26,2025 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Maazimisho ya 22 ya siku ya wahandisi yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo ‘wajibu wa wahandisi kuelekea dira ya maendeleo 2050’.
Amesema miradi isipotekelezwa vyema inaharibu taaluma na kupelekea kupoteza imani kwa wananchi hali inayopelekea taswira mbaya kwa Taifa.
“Naagiza kwa msisitizo mkubwa wahandisi wasiofanya kazi kwa uadilifu na nidhamu bila kufuata viapo vyao wasipewe kazi tena na wachukuliwe hatua kali”,Amesema Ulega.
Aidha imeipongeza ERB kwa kuandaa kongamano hili muhimu kwa mustakabali wa taifa huku akihisii bodi hiyo kuyapeleka mapendekezo yote waliyoyajadili ili serikali iweze kuyashughulikia kwa haraka.
“Nina uhakika kwa makini sana mada zote saba ambazo mlikuwa nazo hivyo hakikisheni mapendokezo yote yalitotokana na mkutano huu yawasilishwe wizarani ili yaweze kufanyiwa kazi kwa maendeleo ya nchi yetu”,Amesema.
Sambamba na hayo amewataka wahandisi kufanyakazi kwa weredi ili malengo ya kitaifa ya dira ya maendeleo ya 2050 yaweze kutimia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ERB Eng.Menye Manga amesema wahandisi 4500 wameshiriki katika maazimisho hayo ambapo wamepata fursa ya kujadili dira ya maendeleo ya 2025 ilipofikia ili kuiendea dira ya maendeleo 2050.
Pia ameongeza kuwa ERB inatarajia kuhitimisha maadhimisho hayo kwa kufanya Marathon yenye lengo kukusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wakike kusoma masomo ya Sayansi ili baadae waweze kuwa wahandisi.
Naye,Mshiriki wa mkutano huo Mhandisi Emmanuel Maloli amesema mkutano huo umewapa fursa ya kubadilishana uzoefu lakini kujadili kwa pamoja fursa ambazo zipo lakini kuijadili dira ya maendeleo 2025 mchango wao kama wahandisi katika kuielekea dira ya maendeleo ya 2050.